Na MWANDISHI WETU, Mahakama-Dar es Salaam
Mahakama ya Tanzania, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) pamoja
na Mabenki mengine nchini wamekutana na kufanya majadiliano kuhusu changamoto za Kisheria
katika Mirathi, usimamizi wa mali za marehemu na uendeshaji wa akaunti maalum ya mirathi, ijulikanayo kama 'Special Mirathi Account.'
Mkutano huo uliohudhuriwa na washiriki wapatao 150 ulifanyika jana tarehe 27 Oktoba, 2026 kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kufunguliwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia-Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa.
Akifungua mutano huo wa majadiliano, Mhe. Mnyukwa, alisema umuhimu wa fedha za mirathi katika familia nyingi nchini zilisababisha kuanzishwa kwa akaunti maalum ya mirathi inayojulikanayo kwa jina la 'Special Mirathi Account' ambayo imesaidia kuimarisha usimamizi wa fedha za mirathi, kuongeza uwazi na kupunguza migogoro inayoweza kujitokeza wakati wa usimamizi na ugawaji wa mali za marehemu.
"Lengo la akaunti hii ni kupokea na kuhifadhi fedha za marehemu ambazo zipo kwenve benki za biashara," amesema Jaji Mnyukwa.
'Special Mirathi Account' ni akaunti inayofunguliwa kupitia mabenki ya biashara na msimamizi wa mirathi aliyethibitishwa na Mahakama.






.jpeg)



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni