Na SHARIFU MOKIWA - Mahakama, Sumbawanga
Chama
cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA), Tawi la Rukwa kimepeleka misaada kwa
wafungwa katika Gereza la Kilimo la Mollo manispaa ya Sumbawanga ikiwa ni sehemu
ya kufanya matendo ya huruma kwa kuwapatia mahitaji muhimu wakati wakiendelea
kutumikia vifungo vyao.
Akizungumza
wakati wa zoezi hilo lililofanyika hivi karibuni, Mwenyekiti wa TMJA Tawi la
Rukwa Mhe. Nickson Temu amesema kuwa, jamii inapaswa kuwakumbuka na kuwajali
wafungwa ikiwa ni pamoja na kuwapelekea mahitaji muhimu kwa matumizi yao wakiwa
gerezani akisisitiza kuwa wafungwa nao ni sehemu ya jamii.
“Tunapaswa
kuwafariji kwa kuja na vitu mbalimbali, sisi sote ni binadamu, gereza halina
mwenyewe, misaada iliyotolewa ni pamoja na sabuni, dawa za meno, mafuta ya
kujipaka, miswaki na zawadi nyingine mbalimbali,” alisema Mhe. Temu.
Amesema
kuwa kuwafikia wafungwa kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali ni moja ya njia ya
kuonesha upendo, ubinadamu na kuwafariji katika kipindi ambacho wapo gerezani.
Zoezi hili ni sehemu ya shughuli za TMJA zinazolenga kushirikiana na jamii,
kuonesha utu na kuwapa faraja wenye uhitaji.
Wanachama
walioshiriki katika zoezi hilo ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo
Sumbawanga, Mhe. Frederick Kapela Manyanda, ambaye pia ni Mlezi wa TMJA Tawi la
Rukwa, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Sumbawanga, Mhe. Pamela
Mazengo, Naibu Msajili Mahakama ya Hakimu Mkazi Sumbawanga Mhe. Kisasila
Saguda, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Sumbawanga Mhe. Lilian
Ndelwa, Katibu wa TMJA Tawi la Rukwa Mhe. Shija Mdadila na wanachama wengine wa
TMJA.
Mwenyekiti
wa TMJA Tawi la Rukwa, Mhe. Nickson Temu kizungumza na maafisa Magereza mara
baada ya kuwasili Gereza la Mollo ikiwa ni pamoja na kuwapelekea wafungwa mahitaji
muhimu kwa matumizi yao wakiwa gerezani.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni