Jumatano, 17 Juni 2026

JAJI KIONGOZI AWATAKA NAIBU WASAJILI WAPYA KUTOBWETEKA

Na HABIBA MBARUKU- Mahakama, Dodoma

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, amewataka Naibu Wasajili wapya 31 kutobweteka na kutowaangusha Viongozi waliowaamini kutekeleza jukumu la utoaji haki kupitia nafasi hizo.

Mhe. Siyani ameyasema hayo baada ya kuwaapisha Naibu Wasajili hao leo tarehe 17 Juni, 2026 katika Ukumbi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama jijini Dodoma.

“Sisi tunaofanya kazi katika Mahakama ya Tanznaia ni Watumishi wa Serikali. Nafasi tunazozipata, ziwe ni nafasi za ajira au nafasi za uongozi kama hizi, ni nafasi ambazo wenzetu wengi zaidi ya milioni 60 hawajabahatika kuzipata, ni nafasi ambazo zinabeba dhamana kubwa, kwa hiyo nitumie nafasi hii kuwasihi sana kutobweteka,” amesisitiza Jaji Kiongozi.

Ameongeza kuwa Naibu Wasajili wa Mahakama ndio injini, moyo na uhai wa Mahakama, hivyo watakapokwenda katika maeneo ambayo watapangiwa watambue kuwa wamebeba matarajio ya wale waliowaamini, kwa niaba ya Watanzania wote.

Amesema kuwa katika Taasisi, zipo changamoto ambazo zimekuwepo kwa muda mrefu na kwamba wao wanatarajiwa kwenda kuzifanyia kazi, huku akibainisha moja ya changamoto inayoikabili Mahakama ni watu kutoridhika na huduma za Mahakama, licha ya uwepo wa takwimu zinazoonesha kuridhika kwa Wananchi, hivyo wanapaswa kuwajibika bila kubweteshwa na takwimu.

Katika hatua nyingine, Mhe. Dkt. Siyani amewataka Naibu Wasajili wapya kufanya kazi bila hofu, huku wakitenda haki, kwa kuzingatia Katiba, Sheria mbalimbali, mila na desturi pamoja na maelekezo ya Viongozi. Amewaeleza kuwa wasiwe na hofu katika kutekeleza majukumu yao kwa sababu wanatarajiwa kwenda kuwahudumia watu, na wanapaswa kuwa na hofu na Mungu pekee ambaye wameapa kwake.

“Msiende kupeleka hofu zenu kazini, mnatarajiwa kwenda kuwahudumia watu na mkiwa na weledi hakuna sababu ya kuwa na hofu, timizeni majukumu yenu vile inavyotarajiwa, hofu itawafanya mkosee, hofu yenu iwe kwa Mungu ambaye mmeapa kwake, msipoweza kudhibiti hali hiyo mtakosea. Katika zama tulizonazo haitajariwi Maaoisa wenye hadhi yenu kufanya makosa yasiyotarajiwa….mkachape kazi,” amesisitiza Jaji Kiongozi.

Ameongeza kuwa miezi sita ijayo itakuwa miezi ya matazamio, hivyo wakienda kubweteka watakosa sifa za kuendelea kuwa Naibu Wasajili kwa sababu uvivu na ukosefu wa weledi ni vitu ambavyo havina nafasi ya kuvumiliwa katika nyakati za sasa na kuwa kila mtu atapimwa kwa haki juu ya namna anavyofanya kazi.

Jaji Kiongozi amewatakiwa kila la heri, huku akiwakumbusha kuiishi kauli mbiu ya Mahakama inayosema, “Uadilifu, Weledi na Uwajibikaji,” akieleza kuwa mambo hayo matatu ndio masingi wa utendaji ulio imara.

Amesema kwamba atakayekosa uadilifu, weledi na kushindwa kuwajibika atakuwa amepoteza sifa ya kuwa Naibu Msajili, hivyo wawe kundi la mageuzi na kundi ambalo litaleta taswira ya kuwa hakukuwa na makosa kwenye kuweka imani kwao.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, akizungumza baada ya kuwaapisha Naibu Wasajili hao leo tarehe 17 Juni, 2026 katika Ukumbi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama jijini Dodoma.

Sehemu ya Naibu Wasajili wapya wakimsikiliza Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, baada ya kuwaapisha.

Sehemu ya Viongozi wa Mahakama na Tume ya Utumishi wakiwa kwenye uapisho huo (juu na chini).


Sehemu ya Wananchi, Watumishi wa Mahakama na Tume ya Utumishi wakiwa kwenye uapisho huo (juu na chini).


Sehemu nyingine ya Wananchi, Watumishi wa Mahakama na Tume ya Utumishi wakiwa kwenye uapisho huo (juu na chini).


Sehemu nyingine ya tatu ya Wananchi, Watumishi wa Mahakama na Tume ya Utumishi wakiwa kwenye uapisho huo (juu na chini).

(Picha na Mary Gwera na Halima Mnete-Mahakama, Dodoma.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.)

 

JAJI MFAWIDHI AHITIMISHA ZIARA YA UKAGUZI MBEYA

Na. MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya.

·        Amepongeza jitihada zinazofanywa kulinda miundombinu ya Mahakama mpya za mwanzo.

·        Amepongeza Serikali za Kata na Vijiji kwa ushirikiano wao katika kuboresha miundombinu ya Mahakama kwa kusaidia ukarabati na hata kutoa Majengo yao kwa matumizi ya Mahakama.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga amehitimisha ziara ya siku kumi za ukaguzi ulioanza mwanzoni mwa mwezi Juni 2026 kwa kutembelea Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzo Mbarali, Chunya, Kyela na Rungwe zilizopo Masjala Ndogo ya Mbeya.

Lengo la ukaguzi huo ni kukumbushana juu ya majukumu ya kila siku, kubaini, mapungufu na changamoto na kuona mapendekezo ya njia sahihi za kukabiliana na changamoto hizo.

Katika vikao mbalimbali vilivyofanyika wakati wa ziara hiyo Mhe. Tiganga aliwasisitiza watumishi kuongeza kasi katika usikilizwaji wa mashauri, kudumisha nidhamu kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kudumisha ushirikiano kazini.

“Ninawapongeza kwa kuendelea kudumisha nidhamu, tuendelee kuchapa kazi, tutunze maadili yetu na ninawapongeza kwa kazi nzuri mnazozifanya na ninawatakieni kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yenu,” alisema Mhe. Tiganga.  

Aidha, Mhe. Tiganga alizipongeza Serikali za Kata na vijiji na wananchi wa maeneo hayo kwa ushirikiano wao mzuri kwa kuisaidia Mahakama kutekeleza majukumu yake ya kutoa haki kwa wakati ikiwa ni pamoja na kusaidia katika harakati za ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Makongorosi iliyopo wilaya ya Chunya na kupatiwa Jengo kwa ajili ya matumizi ya Mahakama ya Mwanzo Ilongo wilayani Mbarali.

Katika ziara hiyo Mhe. Tiganga aliongozana na viongozi mbalimbali wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya ambao ni Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Aziza Temu, Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo, Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Mhe. Zawad Laizer.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (Katikati) akiwa kwenye picha ya Pamoja na watumishi wa mahakama ya Wilaya Rungwe

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (Katikati) akiwa kwenye picha ya Pamoja na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Chunya.

Sehemu ya watumishi wakimsikiliza Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (hayupo pichani) akiongoza kikao katika ziara hiyo ya ukaguzi.


Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya Pamoja na watumishi wa mahakama ya mwanzo Chimala –Mbarali



Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Mhe. Zawadi Laizer, wakipanda mti wa matunda kwa Pamoja katika viunga vya Mahakama ya Mwanzo Madibira- Mbarali.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (watatu kulia) akiwa kwenye picha ya Pamoja na watumishi wa mahakama ya mwanzo Madibira –Mbarali

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akipanda mti wa matunda katika viunga vya Mahakama ya Mwanzo Madibira- Mbarali.

Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti akipanda mti wa matunda katika viunga vya Mahakama ya Mwanzo Ndobo Kyela.

Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo (aliyesimama) akizungumza jambo kwenye moja ya vikao katika ziara hiyo.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akiongoza kikao katika ziara hiyo ya ukaguzi.



Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akisaini kitabu cha wageni na baadae akiongoza kikao katika ziara hiyo ya ukaguzi.



JAJI KIONGOZI AWAAPISHA NAIBU WASAJILI 31 WAPYA WA MAHAKAMA YA TANZANIA

Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, leo tarehe 17 Juni, 2026 amewaapisha Naibu Wasajili 31 wapya wa Mahakama ya Tanzania aliowateua hivi karibuni.

Hafla ya uapisho huo imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Tume ya Utumishi wa Mahakama jijini Dodooma. Uapisho huo unafanya jumla ya Naibu Wasajili wanaohudumu katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani kufikia 108.

Viongozi mbalimbali wa Mahakama, akiwemo Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju, wamehudhuria hafla hiyo. Wengine ni Majaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Amir Mruma na Mhe. Biswalo Mganga, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya na Kaimu Mtendaji Mkuu na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Bw. Victor Kategere.

Wengine ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. George Herbert, Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Chiganga Tengwa, Mtendaji wa Mahakama Kuu Divisheni, Bi. Mary Shirima, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Bw. Leonard Magacha na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu, Mhe. Sundi Fimbo.

Viongozi wengine ni Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Mahakama, Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania, Naibu Wasajili, Watendaji wa Mahakama, Watumishi wa Mahakama na Tume ya Utumishi wa Mahakama, Wazazi, Wenza, ndugu na jamaa wa Naibu Wasajili wapya.

Walioapishwa kwenye hafla hiyo ni Mhe. Agnes Lawrence Mchome kutoka Makao Makuu ya Mahakama, Mhe. Richard Eustace Kabate kutoka Makao Makuu ya Mahakama, Mhe. Janeth Elias Masesa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba, Mhe. Ushindi Solomon Swallo kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mhe. Charles Tumaini Mnzava kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara.

Wengine ni Mhe. Cleofas Frank Waane kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, Mhe. Liad Mohamed Chamshama kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe, Mhe. Hassan Ahmed Makube kutoka Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu, Mhe. Mariam Bakari Lusewa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara na Mhe. Joyce Josephat Mkhoi kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha.

Kwenye orodha wapo pia Mhe. Consolata Peter Singano kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, Mhe. Glory Gabriel Mwakihaba kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga, Mhe. Mkama Ally Abdallah kutoka Mahakama Hakimu Mkazi Moshi, Mhe. Allu Omary Nzowa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida na Mhe. Zabibu Abeid Mpangule kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma.

Wengine ni Mhe. Asha Hassani Waziri kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea, Mhe. Erick Robert Marley kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, Mhe. John Calist Msafiri kutoka Mahakama ya Wilaya katika Kituo Jumuishi Temeke, Mhe. Geofrey Jeremia Mhini kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mhe. Gway Kwaslema Sumaye kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi.

Wapo pia Mhe. Gabriel Patrick Ngaeje kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora, Mhe. Zawadi David Laizer kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Mhe. Martha Mahumbuga kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu, Mhe. Kisasila Malangwa Saguda kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Sumbawanga na Mhe. Erasto Jacobo Philly kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Wengine ni Mhe. Japheti Bwire Manyama kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, Mhe. Is-Haq Bakari Kuppa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Mhe. Samwel Obasi Josiah kutoka Mahakama ya Wilaya Malinyi, Mhe. Jasmini Abdul Athuman kutoka Mahakama ya Wilaya Siha, Mhe. Mwanaheri Kassim Rashid kutoka Mahakama Hakimu Mkazi Tanga na Mhe. Domician Denice Mlashani kutoka Makao Makuu ya Mahakama.

Mhe. Agnes Lawrence Mchome.

Mhe. Richard Eustace Kabate.

Mhe. Janeth Elias Masesa.

Mhe. Ushindi Solomon Swallo.

Mhe. Charles Tumaini Mnzava.

Mhe. Cleofas Frank Waane.

Mhe. Liad Mohamed Chamshama.

Mhe. Hassan Ahmed Makube.

Mhe. Mariam Bakari Lusewa.

Mhe. Joyce Josephat Mkhoi.

Mhe. Consolata Peter Singano.

Mhe. Glory Gabriel Mwakihaba.

Mhe. Mkama Ally Abdallah.

Mhe. Allu Omary Nzowa.

Mhe. Zabibu Abeid Mpangule.

Mhe. Asha Hassani Waziri.

Mhe. Erick Robert Marley.


Mhe. John Calist Msafiri.


Mhe. Geofrey Jeremia Mhini.

Mhe. Gway Kwaslema Sumaye.

Mhe. Gabriel Patrick Ngaeje.

Mhe. Zawadi David Laizer.

Mhe. Martha Mahumbuga.

Mhe. Kisasila Malangwa Saguda.

Mhe. Erasto Jacobo Philly.

Mhe. Japheti Bwire Manyama.

Mhe. Is-Haq Bakari Kuppa. 

Mhe. Samwel Obasi Josiah.

Mhe. Jasmini Abdul Athuman.

Mhe. Mwanaheri Kassim Rashid.


Mhe. Domician Denice Mlashani.

(Picha na MARY GWERA na HALIMA MNETE-Mahakama, Dodoma)