·Atoa ng’ombe kwa watumishi baada ya mashauri 400 kuondoshwa
Na Ahmed Mbilinyi – Mahakama, Bukoba
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Bukoba, Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga ametekeleza ahadi yake ya kutoa zawadi
ya ng’ombe mmoja kwa watumishi wa Mahakama katika Kanda hiyo baada ya kufanikiwa
kupunguza kwa kiasi kikubwa mashauri yanayoendelea mahakamani.
Ng’ombe huyo alichinjwa katika Tamasha la
Ngombe Day lilofanyika mwishoni wa wiki katika eneo la Kabuhara Beach iliyopo
Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera. Mhe. Dkt. Kilekamajenga alitoa ahadi hiyo wakati
ya kikao kazi kilichofanyika mwaka 2021 ambapo Mahakama Kuu Bukoba ilikuwa na mashauri
zaidi ya 900 yaliyokuwa yanaendelea.
Jaji Mfawidhi huyo akaahidi kuwa kama mashauri
hayo yakiPungua hadi kufikia 600 katika Mahakama hiyo atatoa zawadi ya ng’ombe
mmoja. Baada ya kikao hicho timu ya Majaji, Naibu Msajili, Mtendaji wa Mahakama
pamoja na watumishi wote wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba wakaandaa mkakati
pamoja na mpango kazi wa kuwezesha kupunguzwa kwa mashauri hayo.
Katika mkakati huo, majalada asilia
yaliitishwa toka Mahakama za chini, Mabaraza ya Ardhi na Tume ya Usuluhishi na
Uamuzi (CMA) na kisha vikao vya kuondosha mashauri vikaandaliwa na kuendeshwa
na Majaji. Vikao hivyo vilikuwa na mafanikio makubwa ambapo asilimia 98 ya
mashauri yaliyopangwa yalimalizika.
Mwanzoni mwa mwezi Juni 2022 moshi mweupe
ukaanza kuonekana kwa kazi kubwa iliyofanyika, ambapo Mahakama Kuu Bukoba
ikabaki na mashauri 600 yaliyokuwa yakiendelea. Ndipo Mhe. Dkt. Kilekamajenga
akatoa tamko la kutoa ng’ombe kutimiza ahadi yake.
Kufuatia hatua hiyo, kamati ya maandalizi
ikaundwa kuratibu tamasha, ambalo kushirikisha michezo mbalimbali, wakati huo huo
kazi ya kushughulikia mashauri ikiwa inaendelea kufanyika na hadi kufikia mwanzoni
mwa mwezi Septemba 2022, Mahakama Kuu Bukoba ilibaki na mashauri yanayoendelea 495
tu.
Hatimaye tamasha likafanyika huku
watumishi wa Mahakama wakiburudika na nyama iliyochinjwa pamoja na michezo
mbalimbali iliwemo mashindano ya kula nyama na kunywa soda, Mpira wa Miguu kwa Wanawake
na Wanaume huku timu husika zikiganyika kwa mashabiki wa Simba na Yanga.
Kadhalika, kulikuwepo na mbio za mita mia (100), mbio za kupokezana vijiti,
mashindano ya kuogelea pamoja na mchezo wa meza (pool table).
💪🏾💪🏾💪🏾♨️♨️♨️
JibuFuta