Jumatano, 17 Juni 2026

JAJI KIONGOZI AWAAPISHA NAIBU WASAJILI 31 WAPYA WA MAHAKAMA YA TANZANIA

Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, leo tarehe 17 Juni, 2026 amewaapisha Naibu Wasajili 31 wapya wa Mahakama ya Tanzania aliowateua hivi karibuni.

Hafla ya uapisho huo imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Tume ya Utumishi wa Mahakama jijini Dodooma. Uapisho huo unafanya jumla ya Naibu Wasajili wanaohudumu katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani kufikia 108.

Viongozi mbalimbali wa Mahakama, akiwemo Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. George Masaju, wamehudhuria hafla hiyo. Wengine ni Majaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Amir Mruma na Mhe. Biswalo Mganga, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya na Kaimu Mtendaji Mkuu na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Bw. Victor Kategere.

Wengine ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. George Herbert, Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Chiganga Tengwa, Mtendaji wa Mahakama Kuu Divisheni, Bi. Mary Shirima, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Bw. Leonard Magacha na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu, Mhe. Sundi Fimbo.

Viongozi wengine ni Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa Mahakama, Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania, Naibu Wasajili, Watendaji wa Mahakama, Watumishi wa Mahakama na Tume ya Utumishi wa Mahakama, Wazazi, Wenza, ndugu na jamaa wa Naibu Wasajili wapya.

Walioapishwa kwenye hafla hiyo ni Mhe. Agnes Lawrence Mchome kutoka Makao Makuu ya Mahakama, Mhe. Richard Eustace Kabate kutoka Makao Makuu ya Mahakama, Mhe. Janeth Elias Masesa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba, Mhe. Ushindi Solomon Swallo kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mhe. Charles Tumaini Mnzava kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara.

Wengine ni Mhe. Cleofas Frank Waane kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, Mhe. Liad Mohamed Chamshama kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe, Mhe. Hassan Ahmed Makube kutoka Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu, Mhe. Mariam Bakari Lusewa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara na Mhe. Joyce Josephat Mkhoi kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha.

Kwenye orodha wapo pia Mhe. Consolata Peter Singano kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, Mhe. Glory Gabriel Mwakihaba kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga, Mhe. Mkama Ally Abdallah kutoka Mahakama Hakimu Mkazi Moshi, Mhe. Allu Omary Nzowa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida na Mhe. Zabibu Abeid Mpangule kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma.

Wengine ni Mhe. Asha Hassani Waziri kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea, Mhe. Erick Robert Marley kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, Mhe. John Calist Msafiri kutoka Mahakama ya Wilaya katika Kituo Jumuishi Temeke, Mhe. Geofrey Jeremia Mhini kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mhe. Gway Kwaslema Sumaye kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi.

Wapo pia Mhe. Gabriel Patrick Ngaeje kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora, Mhe. Zawadi David Laizer kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Mhe. Martha Mahumbuga kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu, Mhe. Kisasila Malangwa Saguda kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Sumbawanga na Mhe. Erasto Jacobo Philly kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Wengine ni Mhe. Japheti Bwire Manyama kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, Mhe. Is-Haq Bakari Kuppa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni, Mhe. Samwel Obasi Josiah kutoka Mahakama ya Wilaya Malinyi, Mhe. Jasmini Abdul Athuman kutoka Mahakama ya Wilaya Siha, Mhe. Mwanaheri Kassim Rashid kutoka Mahakama Hakimu Mkazi Tanga na Mhe. Domician Denice Mlashani kutoka Makao Makuu ya Mahakama.

Mhe. Agnes Lawrence Mchome.

Mhe. Richard Eustace Kabate.

Mhe. Janeth Elias Masesa.

Mhe. Ushindi Solomon Swallo.

Mhe. Charles Tumaini Mnzava.

Mhe. Cleofas Frank Waane.

Mhe. Liad Mohamed Chamshama.

Mhe. Hassan Ahmed Makube.

Mhe. Mariam Bakari Lusewa.

Mhe. Joyce Josephat Mkhoi.

Mhe. Consolata Peter Singano.

Mhe. Glory Gabriel Mwakihaba.

Mhe. Mkama Ally Abdallah.

Mhe. Allu Omary Nzowa.

Mhe. Zabibu Abeid Mpangule.

Mhe. Asha Hassani Waziri.

Mhe. Erick Robert Marley.


Mhe. John Calist Msafiri.


Mhe. Geofrey Jeremia Mhini.

Mhe. Gway Kwaslema Sumaye.

Mhe. Gabriel Patrick Ngaeje.

Mhe. Zawadi David Laizer.

Mhe. Martha Mahumbuga.

Mhe. Kisasila Malangwa Saguda.

Mhe. Erasto Jacobo Philly.

Mhe. Japheti Bwire Manyama.

Mhe. Is-Haq Bakari Kuppa. 

Mhe. Samwel Obasi Josiah.

Mhe. Jasmini Abdul Athuman.

Mhe. Mwanaheri Kassim Rashid.


Mhe. Domician Denice Mlashani.

(Picha na MARY GWERA na HALIMA MNETE-Mahakama, Dodoma)


 

 

JAJI KISANYA AKABIDHIWA RASMI OFISI MASJALA NDOGO MWANZA

Na. REHEMA AWET – Mahakama, Mwanza

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mwanza imeingia katika awamu mpya ya Uongozi leo tarehe 17 Juni, 2026, baada ya hafla ya makabidhiano ya Ofisi ya Jaji Mfawidhi kufanyika.

Hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi ya Jaji Mfawidhi Masjala Ndogo ya Mwanza, ilishuhudiwa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Dkt. Ntemi Kilekamajenga akikabidhi rasmi kijiti cha uongozi kwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ephery Kisanya.

Makabidhiano hayo yalijikita katika kukabidhi majukumu ya kiutawala, nyaraka mbalimbali za ofisi, na taarifa muhimu za utendaji kazi, zote zikiwa na lengo la kuhakikisha mwendelezo wa utoaji wa huduma za kimahakama na usimamizi wa shughuli za Mahakama katika Masjala Ndogo hiyo ya Mwanza.

Akizungumza katika hafla hiyo, Jaji Dkt. Ntemi Kilekamajenga alimpongeza Jaji Ephery Kisanya kwa kukabidhiwa majukumu hayo na kumtakia mafanikio katika utekelezaji wake.

Kwa upande wake, Jaji Ephery Kisanya aliahidi kuendesha ofisi hiyo kwa weledi, kuendeleza ushirikiano baina ya wafanyakazi, na kuimarisha upatikanaji wa huduma za haki kwa wananchi wa Masjala hiyo ya Mwanza.

Makabidhiano hayo yanaashiria mwanzo wa awamu mpya ya uongozi katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mwanza, huku yakisisitiza dhamira ya kuendeleza ufanisi, uwazi na ubora katika utoaji wa huduma za Mahakama kwa wananchi.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mwanza ambaye amehama Kituo Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga (kushoto) akimkabidi Ofisi Jaji Mfawidhi Mpya wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Mwanza Mhe. Ephery Kisanya (kulia).

Jaji Mfawidhi Mpya wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Mwanza Mhe. Ephery Kisanya akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili ofisini Masjala Ndogo.

Jumanne, 16 Juni 2026

MAHAKAMA SUMBAWANGA YAFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MAGEREZA

Na. SHARIFU MOKIWA – Mahakama, Sumbawanga

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Sumbawanga Mhe. Frederick Kapela Manyanda amefanya ziara ya kutembelea Gereza la Mahabusu Sumbawanga na Gereza la Mollo la Kilimo kwa ajili ya kusikiliza changamoto mbalimbali za wafungwa na Mahabusu wa magereza hayo, ikiwa ni zaira ya ukaguzi wa kawaida katika kipindi cha Juni, 2026.

Akiwasilisha taarifa fupi ya Gereza Kuu la Mahabusu Sumbawanga jana tarehe 15 Juni, 2026 Mkuu wa Gereza Mahabusu Sumbawanga Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Ally M. Abdallah  alieleza hali za wafungwa na mahabusu waliopo gerezani hapo.  

Mhe. Manyanda alipata fursa ya kukutana na Wafungwa na Mahabusu ambao waliwasilisha changamoto zao kwa viongozi mbalimbali wa Mahakama na wadau wengine wa haki jinai alioambatana nao,

Akijibu hoja mbalimbali Mhe. Manyara alielekeza kuharakishwa kwa hatua za upelelezi wa mashauri mbalimbali yanayohusisha Watoto ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wakati mapema ipasavyo na wahusika wanapata huduma stahiki kwa mujibu wa sheria.

Aidha, Mhe. Mnyanda, alielekeza kubainishwa kwa changamoto zinazo kwamisha mwenendo wa mashauri ya jinai na kuzitaka kamati za haki jinai kushirikiana kwa karibu katika kuzitatua pamoja na kusukuma mbele mashauri yaliyopo ili kupunguza mlundikano wa mashauri.

Katika risala yao wafungwa na mahabusu katika Gereza la Mahabusu Sumbawanga waliweza kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili gerezani hapo mbele ya Mhe. Manyanda. Aidha, Mhe. Manyanda aliahidi kuzishughulikia changamoto zote zilizowasilishwa katika risala zao na zile ambazo zipo nje ya uwezo kuziwasilisha katika mamlaka husika.

Kwa upande wake, Mkuu wa Gereza la Mahabusu Sumbawanga ACP Ally M. Abdallah alitoa shukurani zake kwa ujio wa ziara hiyo, kwa kuwa umekuwa na tija kubwa kwao kwa kutoa fursa kadhaa ikiwemo matendo ya huruma na kushughulikia suala la kupunguza mlundikano wa mahabusu gerezani hapo.

Katika ziara hiyo Mhe. Manyanda aliambatana na Viongozi mbalimbali wa Mahakama akiwemo Mtendaji Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Sumbawanga  Bw. Machumu Essaba, Msaidizi wa Sheria, Mkuu wa upelelezi Mkoa, Kaimu Hakimu Mkazi Mkoa, Hakimu Mfawidhi wa Wilaya, Afisa Ustawi  Mkoa, Mkuu wa Mashtaka Mkoa, Mwakilishi wa Kamanda Takukuru Mkoa, Ofisi ya Upelelezi Mkoa, Afisa Huduma na Uangalizi, Afisa Uhamiaji Mkoa, Mkuu wa Magereza Mkoa na wadau wengine wa Haki jinai.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Sumbawanga Mhe. Frederick Kapela Mnyanda (katikati) akiwa pamoja na wadau wengingine wa haki jinai wakiwa katika gereza la kilimo Mollo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Sumbawanga Mhe. Frederick Kapela Manyanda (kushoto) akipokea risala kutoka kwa Afisa wa Jeshi la Magereza.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Sumbawanga Mhe. Frederick Kapela Manyanda (mbele ya picha kulia) akiwasili katika ukaguzi wa Gereza la Mahabusu Sumbawanga. 

(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha-Mahakama)

  

USHIRIKIANO KAZINI NI NYENZO MUHIMU KATIKA KUBORESHA UTENDAJI KAZI

Na. MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga amesema ushirikiano na mahusiano mazuri kazini ni nyenzo muhimu katika kuboresha utendaji kazi ujumbe huo ameutoa wakati alipotembelea Mahakama zilizopo Mbeya Mjini ikiwa ni kuanza kwa ukaguzi wa kawaida warobo ya nne ya mwaka 2025/2026.

Ziara hiyo iliyofanyika mwanzoni mwa mwezi Juni, kwa kutembelea sehemu ya Mahakama kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa katika Mahakama hizo na alipata wasaa wa kuzungumza na watumishi wa Mahakama hizo katika vikao vya pamoja vilivyofanywa wakati wa ziara hiyo.

Akizungumza katika vikao hivyo, vilivyofanyika katika ukaguzi huo, Mhe. Tiganga alisisitiza kudumisha nidhamu, ushirikiano na mahusiano mazuri mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji wa watumishi katika kupanga mambo mbalimbali ya kiutendaji.

“Nasisitiza kudumisha nidhamu na mahusiano mazuri kazini, tuishi kwa upendo na tujifunze kuvumiliana pale inapotokea kupishana baina yetu, tuepuke mambo ambayo hayana ulazima Kutugawa, tusitengeneze ugumu wa kazi kwa kuwekeana vinyongo na vikwazo baina yetu. Pia nawakumbusha kuhusu umuhimu wa ushirikishwaji wa watumishi katika kupanga mambo mbalimbali ya kiutendaji katika ofisi zetu,” alisema Mhe. Tiganga katika ziara yake hiyo.

Mhe. Tiganga aliongezea kwa kusisitiza umuhimu wa kutunza na kulinda rasilimali za Mahakama na kuzingatia hasa vipaumbele vya ofisi kulingana na bajeti zenu kila fedha za matumizi ya ndani zinapoletwa.

Aidha Mahakimu Wafawidhi wa Vituo hivyo alivyotembelea walitoa shukrani zao kwa ziara hiyo na kuahidi kuwa wako tayari kutekeleza yale yote waliyoelekezwa na viongozi wao ili kuboresha utendaji kazi katika vituo vyao na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Aidha, kupitia taarifa mbalimbali zilizowasilishwa na Mahakimu Wafawidhi wa Vituo mbalimbali alivyotembelea zilieleza juu ya usimamizi wa rasilimali mbalimbali zilizopo, utekelezaji wa majukumu ikiwa ni pamoja na hali ya mashauri katika vituo hivyo.

Sambamba na hilo, Taarifa hizo zilieleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika vituo vyao ambapo wengi wao walieleza hasa kuhusu uhaba wa watumishi hasa kada ya walinzi, uchakavu wa vyombo vya usafiri na uchakavu wa majengo hasa kwa Mahakama za mwanzo.

Katika ziara hiyo Mhe. Tiganga, aliambatana na viongozi mbalimbali wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, akiwemo Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti, Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo, Afisa Utumishi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bw. Moses Luoga na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Mhe. Zawadi Laizer.

 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Watoto Mbeya.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (katikati) akiwa ndani ya Ofisi ya Mahakama ya hakimu mkazi Mbeya, kulia ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Majala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo na kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Mhe. Zawadi Laizer.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (katikati walioketi mbele). akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, walioketi mbele, kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti na kushoto ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (watatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya wilaya Mbeya katika ukaguzi huo, wanne kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbeya, Mhe. Tedy Mlimba.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akizungumza kwenye moja ya vikao vilivyofanyika katika ziara hiyo.

Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti (katikati) akizungumza jambo kwenye moja ya vikao katika ziara hiyo.

Sehemu ya Watumishi wakimsikiliza Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (hayupo pichani) akizungumza kwenye moja ya vikao vilivyofanyika katika ziara hiyo.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (aliyekaa mbele)akizungumza kwenye moja ya vikao vilivyofanyika katika ziara hiyo.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (aliyekaa mbele)akizungumza kwenye moja ya vikao vilivyofanyika katika ziara hiyo.

(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha-Mahakama)

MAHAKAMA KUU GEITA YAMUAGA JAJI MFAWIDHI MHINA

Na DOTTO NKAJA –Mahakama,  Geita

Uongozi na Watumishi wa Mahakama Kuu Masjla Ndogo Geita hivi karibuni walifanya hafla ya kumuaga aliyekuwa Jaji Mfawidhi, Mhe. Kevin Mhina, kufuatia uhamisho wake wa kwenda kutekeleza majukumu katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara.

Hafla hiyo ilifanyika Juni 10, 2026, katika Viwanja vya Mahakama Kuu Geita. Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mhina aliwashukuru wote kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha utumishi wake. Alisema amefurahishwa na maandalizi ya hafla hiyo na kupongeza mshikamano ulioonyeshwa na Watumishi.

Aidha, aliwahimiza kuendelea kuzingatia maadili ya kazi, ushirikiano, utu na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Pia alisisitiza umuhimu wa kuendeleza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuimarisha utoaji wa huduma za haki na kuifanya Mahakama Geita kuwa mfano katika matumizi ya teknolojia ndani ya Mhimili wa Mahakama.

Kwa niaba ya watumishi, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Griffin Mwakapeje, alimpongeza Mhe. Mhina kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Mahakama Geita, hususan katika kusimamia uanzishwaji wa Masjala ya Mahakama Kuu Geita.

Alisema uongozi wake wenye maono, uthabiti na kujitolea umechangia kuimarika kwa huduma za Mahakama na kuongeza ufanisi katika utoaji wa haki kwa Wananchi.

Naye Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Geita, Mhe. Fredrick Lukuna, alimpongeza Mhe. Mhina kwa juhudi zake katika kuhamasisha na kuendeleza matumizi ya TEHAMA katika shughuli za Mahakama.

Alisema maarifa, uongozi na moyo wake wa kusaidia wengine vimechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha matumizi ya teknolojia katika uendeshaji wa mashauri, usikilizaji wa kesi na shughuli za kiutawala.

Kwa upande wake, Mtendaji wa Mahakama Geita, Bi. Masalu Kisasila, alisema Mhe. Mhina ameacha alama ya uongozi bora kutokana na malezi ya kitaaluma, msimamo wake katika kusimamia maadili na weledi kazini, pamoja na juhudi zake za kuwajengea uwezo Watumishi.

Alibainisha kuwa uongozi wake umeweka msingi imara wa uwajibikaji, uadilifu na heshima katika mazingira ya kazi, hali iliyochangia kuimarika kwa utendaji wa Mahakama Geita.

Hafla hiyo ilihitimishwa kwa Viongozi na Watumishi mbalimbali kutoa salamu za shukrani na pongezi kwa Mhe. Mhina kwa mchango wake katika maendeleo ya Mahakama Geita, huku wakimtakia mafanikio zaidi katika majukumu yake mapya.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Mhe. Kevin Mhina, akitoa shukurani.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Mhe. Kevin Mhina akimulishakeki Jaji wa Mahakama Kuu Geita, Mhe. Griffin Mwakapeje.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Mhe. Kevin Mhina akiwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Geita, Mhe. Fredrick Lukuna Pamoja na Mtendaji wa Mahakama Geita, Bi. Masalu Kisasila.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Mhe. Kevin Mhina akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama Kuu Geita.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Mhe. Kevin Mhina akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Mhe. Kevin Mhina akiwa katika picha ya Pamoja na watumishi wa mahakama ya wilaya Geita.

Picha Namba 7. Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Geita, Mhe Kevin Mhina akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Chato.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Mhe. Kevin Mhina akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Bukombe.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Mhe. Kevin Mhina akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Nyanghwale.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara, Mhe. Kevin Mhina akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Mbogwe.

 Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma.